Twitter

Twitter Buttons

Monday, 26 August 2013

Jicho Kwa Mafahali Watatu: Yanga Mteremko...Simba na Azam Hesabu.


                                  
Msimu wa 2013/2014 wa ligi kuu ya Vodacom ndio umeanza rasmi kwa mechi za raundi ya kwanza kuchezwa mwisho wa juma. Mechi za kwanza zimeshuhudia mabingwa watetezi , Yanga wakiibuka na ushindi mkubwa zaidi. Chini ya kocha wao Mholanzi Ernie Brandts waliiporomoshea kipigo cha mbwa mwizi timu ya Ashanti United iliyopanda daraja msimu huu.

Yanga ilitarajiwa kushinda lakini si kwa kutoa kipigo cha 5-1, hili halikutarajiwa na wengi hasa ukizingatia kuwa Ashanti walionekana kuwa wamejikakamua kwa maandalizi ya kutosha. Ashanti walipiga hatua hadi ya kufanya ziara nje ya nchi katika kujiandaa na ligi. Wengi tulitarajia kuwa watatoa ushindani kwa Yanga. Kinyume na matarajio wameambulia kipigo ambacho kinaweza kuwa kipigo kikali zaidi katika msimu mzima.

Ingawa  msimu ndio umeanza, lakini Yanga wanaonekana kuwa kamili sana ukilinganisha na wapinzani wao. Ukamili wa Yanga hautokani na kuwa na wachezaji bora kulinganisha na Simba na Azam, la hasha, wapo bora kutokana na mbinu za kocha wao. Kwa mchezaji mmoja mmoja, Simba na Azam wanaweza kuwa bora kuliko Yanga na pia wanaweza kuendelea kutoa wachezaji wengi katika timu za taifa. Japo ni mapema sana lakini tunaweza kushuhudia filamu ya msimu uliopita ya wachezaji wa Simba na Azam kutamba katika timu ya taifa huku Yanga wakitesa kwenye mbio za ubingwa. 

Ubora wa Yanga unatokana na mbinu za kocha wao kucheza mchezo wa kushambulia moja kwa moja. Wako ‘direct’, wanatumia pasi chache kulifikia lango la adui kulinganisha na wapinzani wao, Azam na Simba. Yanga wana wachezaji wengi wenye kasi, kuanzia Msuva, Juma Abdul, Salum Telela hadi ingizo jipya Mrisho Ngassa. Hawa ni hatari hasa wakikuta walinzi waliozubaa. Ni tofauti na Azam na Simba ambao wanapendelea zaidi kumiliki mpira hasa kwenye maeneo yasiyo na madhara kwa adui.

Ikumbukwe kuwa kocha Ernie Brandts alikuta ligi ya msimu uliopita imekwishaaanza licha ya kuwa aliweza kubeba ubingwa. Msimu huu Yanga inaweza kuwa hatari zaidi kwa kuwa kocha ameanza na timu toka mwanzo na hivyo kupata muda mwafaka wa kushughulikia mapungufu.
Jambo la hatari zaidi kwa wapinzani  wenye ndoto za kuwapokonya ubingwa Yanga ni jeshi la mashabiki lililo nyuma ya Yanga hasa kwa kasi walioanza nayo. Hakuna shaka kuwa Yanga inaongoza kuvutia mashabiki uwanjani na hasa timu yao inapokuwa katika wimbi la ushindi basi mashabiki wake huongezeka maradufu.

Azam anaanzia ugenini mechi tatu za kwanza,ni ratiba ngumu kwake. Ameanza kwa sare na Mtibwa Sugar kisha anamfuata Rhino Rangers kabla ya kumalizana na Kagera Sugar huko Kaitaba. Simba naye anaanzia ugenini mechi mbili za kwanza, ameanza kwa sare dhidi ya Rhino kasha anawafuata wanajeshi wengine, JKT Oljoro kabla ya kupambana na Mtibwa Sugar nyumbani. Kwa haraka haraka utaona kuna hatari ya Azam na Simba kujikuta wakiwa nyuma ya Yanga kwa pointi kadhaa ndani ya raundi tatu tu za mwanzo. Yanga wao wanaanzia nyumbani mechi mbili za kwanza,wamemsarambatuisha Ashanti, Coastal anawafuata kabla ya wao kusafiri kwa kuku mgeni wa ligi, Mbeya City.

Simba na Azam itawabidi kuchanga karata zao vizuri ili wasije kujikuta wanatimuliwa vumbi  baada ya raundi chache tu za mwanzoni. Yanga wakitoka, wapinzani wahesabu maumivu. Ni hatari kuwaacha Yanga watangulie mbele, hasa Yanga hii chini ya mholanzi.

Friday, 23 August 2013

Ligi Kuu 2013/2014; Ndoto za Ubingwa Azam, Na Kamari ya Stewart Hall

                              


Licha ya uwekezaji wa kiwango kikubwa , ubingwa wa ligi kuu umeendelea kuwa simulizi ya ‘msimu ujao’ kwa vijana wa Chamazi. Kwa misimu miwili mfululizo, wamekaribia sana kutwaa ubingwa lakini mara zote wamefia ufuoni na kuwaacha wakongwe Simba na Yanga wakishangilia. Kwenye msimu huu mpya, Kwa mara nyingine watajitupa kwenye ulingo kupigania ubingwa wa ligi kuu. Licha ya kushiriki michuano ya Afrika, akili na nguvu zao zitakuwa zimeelekezwakwenye ligi kuu kuhakikisha wanapambana mpaka dakika ya mwisho kuchukua ubingwa. Ndio kombe la msingi zaidi  kwao licha ya kuwa kombe la shirikisho ni kubwa zaidi. Kombe la shirikisho litabaki kuwa mazoezi ya ndoto zao za siku za usoni.

Azam,licha ya kuhesabika kama moja ya vigogo vya soka nchini, bado hawajaingia rasmi katika historia ya vigogo wa soka nchini. Ubavu wao wa fedha unaweza kuwa umewapa heshima ya kuitwa vigogo lakini kihistoria wao bado ni kinda kwa Coastal Union, Mtibwa Sugar na Pamba . Hivi ni baadhi tu ya vilabu ambavyo vipo katika kumbukumbu za historia za ubingwa Tanzania. Kwa sasa Azam ni vigogo lakini ni kofia ya ubingwa tu ndio itawapa heshima na hadhi ya kuitwa vigogo wa soka nchini. Jeuri ya pesa inaipa klabu ukuu wa muda tu, ubingwa unatoa hadhi ya kihistoria. Mwisho wa siku, historia huandikwa na mabingwa tu. 

Azam waliingia kambini mapema, wamefanya ziara ya siku kumi huko Afrika Kusini Pamoja na mikakati mingine katika jitihada zao za kujifua kwa ajili ya mbio za ubingwa wa ligi kuu. Licha ya yote hayo,kamari kubwa zaidi waliyocheza ni kutosajili wachezaji wapya kwa msimu huu. Ni ngumu kuamini kuwa  ni mkakati wa utawala kuamua kutosajili hasa baada ya kukaribia sana kutwaa ubingwa msimu uliopita. Kwa namna yoyote ile utakuwa ni uamuzi wa kocha wao. 

Inawezekana kocha Stewart Hall ameamua kutengeneza mshikamano na umoja katika kikosi kuliko kusajili wachezaji wapya ambao watachukua muda kuelewana. Ameamua kuwafyeka baadhi ya wachezaji ambao ameona hatawahitaji na kupandisha chipukizi kadhaa. Kati ya waliokumbwa na panga ni Pamoja na kiungo mshambuliaji, Abdi Kassim, Abdulhalim Humud na kipa Munishi. Jambo la kustaajibisha ni kuwa wawili kati ya watatu waliotemwa,Munishi na Humud wameibukia kwa wapinzani wao wakubwa, Simba na Yanga. Kama filamu ya kejeli hivi, Munishi katika mechi yake ya kwanza aliizuia Azam kuchukua ubingwa wa kombe la ngao ya jamii kwa kuokoa hatari zote zilizoelekezwa langoni mwake.

Humud, kiungo matata, ambaye kama akitulia na kuamua kucheza mpira Azam wanaweza kujikuta wakimwaga machozi kwa kuwapa silaha wapinzani wao. Kwenye biashara za kuwania ubingwa ni kosa kubwa kumpa unafuu adui yako lakini Azam ni kama wamefanya hivyo kwa kuwaimarisha Simba na Yanga. Suala la kutemwa kwa Abdi Kassim lina utata zaidi hasa baada ya kila upande kutoa kauli tofauti. Kwa waliofuatilia ligi msimu uliopita watagundua kuwa licha ya kuonekana kuwa umri umemtupa mkono bado Babbi alitoa mchango mkubwa wa magoli.

Bila ya Abdi Kassim na huku Humphrey Mieno akiwa majeruhi, Azam wanaweza kujikuta wakiwa hawana kiungo mshambuliaji wa kuwasidia ufungaji. Ukichungulia kwa wapinzani wao, Simba na Yanga utagundua wako vyema kwa kuwa na Amri Kiemba na Haruna Niyonzima. Kuna wakati washambuliaji wa Yanga walikuwa likizo ya kufunga lakini Niyonzima na Nizar Khalfan wakabeba majukumu vizuri .Yanga ilijikuta ikiambulia ushindi wa bao moja mfululizo kutokana na viungo washambuliaji kuwasaidia washambuliaji na hivyo kujikuta timu ikisonga mbele bila kuyumba. Kwa upande wa Simba, mchango wa mabao wa Amri Kiemba unajulikana.Kwa misimu miwili mfululizo sasa, Kiemba amekuwa msaada mkubwa kwa Simba kutokana mabao anayofunga. Kwa jicho la haraka, utagundua Azam hawana mtu wa hivyo msimu huu. Wamemtema Abdi Kassim na kushindwa kuziba pengo lake.

Ni jambo la kusubiri na kuona mwisho wa msimu utakuaje licha ya kuwa kuna dirisha dogo la usajili baada ya mzunguko wa kwanza. Stewart anaweza kusajili kipindi hicho lakini kama watakuwa wamevurunda na kuachwa na Simba au Yanga basi itabidi wasahau ubingwa kwa mara nyingine.Simba na Yanga wakikutanguliza ni ngumu sana kuwakamata kwa kuwa mashabiki wao wanakuwa nyuma yao kuwahamasisha. Kwa kucheza kamari ya kutosajili Stewart Hall anaweza kuibuka shujaa au kuishia kufungasha virago na kurudi katika fukwe baridi za vya Uingereza.

Thursday, 22 August 2013

Time For Tanzanian Referees To Either Shape Up Or Ship Out


                         

More than thirteen years have passed since the last time a Tanzanian referee officiated an AFCON tournament match. The legengadary Omar Abdikadir officiated in the 1998 AFCON edition in Burkina Faso. Apparently, Abdikadir blundered so much that Tanzanian referees have since never been considered to officiate in subsequent CAF tournaments. Perhaps that earned our referees a biased stigma but the current lot of local referees does not inspire confidence of doing a better job.

Football officials were once again in the spotlight during Saturday’s memorable Community Shield cup tie between Azam and Young Africans. Though there was no official complaint raised one could see both coaches exasperated with every poor call from the match officials. Stewart Hall, the Azam tactician, in particular cut a frustrating figure in the touch line as he tried to grasp with the numerous bad calls from the officials. 

During the first half, the match was stopped for more than six minutes as Yanga goalkeeper, Ally Mustapha was being treated by medical attendants on the field. Surprisingly, as the first half drew to a close, the fourth official signaled that at least four minutes of stoppage time would be played. Many expected the centre official, Oden Mbaga to at least allow play for five minutes to compensate for time lost while Mustapha was being given medical attention. To the dismay of many, Oden Mbaga blew his whistle for half-time after barely four minutes of additional time. Two minutes might not be enough reason to crucify the referee but it is this kind of little mistakes that hinders our referees’ progress in officiating big matches in the international stage. Who is going to trust our officials with big matches if they cannot even observe the correct time?

Another incident that highlighted our football officials’ ineptitude came in the 70th minute involving Azam striker,John Bocco and Young Africans Rwandan import defender, Mbuyu Twitte. The Rwandan import made a cynical sliding tackle on Bocco that left the striker reeling in pain.  Twitte, a cheeky defender, got the ball cleanly but cynically booted Bocco on the shin forcing him to be substituted. Again to the dismay of many, Twitte’s cynical tackle went unpunished as Bocco dropped out of the game. The match official did not even bother to award a free kick, it was game on as if nothing had happened.

For the first time many local premier league matches would be beamed live to a wider audience after the signing of a deal between Azam Tv and Tanzania Premier league committee.  State of the art outside broadcasting vehicle (OB) will be used to cover games. These are 12-camera supported OBs that can fully record every angle and thus will expose our officials who have been blamed for making poor calls. With the introduction of such state of the art technology, more and more of our poor referees will be on the spotlight. It is time they either shape up or ship out.



Saturday, 17 August 2013

Yanga Vs Azam Community Shield Cup; Third Against First

 



 Having twice emerged first runner up to both Simba and Yanga in the past two seasons, Azam have nowhere to run but going for the league title this season. The only way up is the title, nothing less, anything less than that would be a disappointment to the ambitious Chamazi outfit. This is their sixth season since they got promoted and seventh year anniversary; they have a chance to make their title ambition clear as they face Young Africans in the community shield cup. Last season they came within a whisker of winning their first shield cup only to be cruelly denied by a late 30-metre bullet winning goal from Kazimoto. Goals from the lethal duo of Bocco and Ivorian hitman, Tchetche had given them a 2-0 lead only to blow it away in the second half. Simba Ghanaian import, Daniel Akuffo converted from the spot kick after Said Morad handled the ball, to reduce their lead to 2-1. Then Emmanuel Okwi leveled the score before Kazimoto scored the winning goal for Simba.

They are facing Young Africans, a side which has handed them three consecutive defeats. In three past matches against them, Azam have not scored a goal conceding five in the process. Yanga did not only win the league ahead of Azam, they did a double, winning 2-0 and 1-0 in the first and second rounds respectively. To further compound misery, Yanga stopped them from being crowned Cecafa regional champions by beating them 2-0 in the final. 

They have stuck with virtually the same side, only promoting three junior players from their academy. Nevertheless they still possess enough power within their ranks to win their first community shield cup. Stewart Hall has been around long enough to realize going into the match, Yanga have the momentum and there is something profound the Dutch tactician, Ernie Brandts has injected in the Jangwani side. While Azam are fresh from a South Africa pre-season tour where they trained with the more tactical astute PSL clubs, Yanga have had a relative low pre-season preparation in Tanzania.

Yanga will not only be seeking to continue their recent dominance over Azam but also winning a record third community shield cup. They won the inaugural edition in 2001 and repeated the feat a decade later, 2011. Azam know a loss will be a psychological blow to their title ambitious. Given Yanga massive fan base, a victory will propel large attendance turn outs in league matches that will give Yanga a big advantage over other contenders, Azam included. Will the community shield cup virgins, Azam do it?





Yanga Vs Azam Factfile/Stats

Results Summary


Date                   Place      Round    Home                     Away                          Tournament    
23/02/2013         Dar         R18         Yanga      1-0       Azam                Ligi kuu Bara 12/13           
04/11/2012         Dar         R5           Azam       0-2       Yanga               Ligi kuu Bara 12/13
28/07/2012         Dar        Final       Yanga        2-0       Azam               Kagame cup 2012
10/03/2012         Dar         R19        Yanga       1-3       Azam               Ligi kuu Bara 11/12          
18/09/2011         Dar         R6            Azam     1-0      Yanga                Ligi kuu Bara 11/12          
30/03/2011         Dar         R20          Yanga     2-1      Azam                Ligi kuu Bara 10/11          
24/10/2010         Dar         R9            Azam     0-0     Yanga                 Ligi kuu Bara 10/11          
07/03/2010         Dar         R19          Yanga     2-1     Azam                 Ligi kuu Bara 09/10          
17/10/2009         Dar         R8            Azam     1-1     Yanga                 Ligi kuu Bara 09/10          
08/04/2009         Dar         R19          Yanga     2-3     Azam                 Ligi kuu Bara 08/09          
15/10/2008         Dar         R8           Azam       1-3     Yanga                Ligi kuu Bara 08/09 
  

                           P        W          L      D   GF       GA
Yanga                 11       6            3      2      16     11
Azam                  11       3            6      2      11    16